babu wa loliondo ameanza kuhofia maisha yake baada ya kuwepo taarifa kuwa kuna watu wanachukizwa na anchokifanya na hivyo wanatarget kumdhulu. babu amenukuliwa akisema hivi,
"Wanachukia kusikia natoa tiba ya magonjwa hapa, sasa wanajipanga kila siku kuniangamiza ,lakini Mungu ananilinda kila kona sambamba na vyombo vya dola vilivyopo hapa na hawataniweza hadi Mungu anichukue mwenyewe,"
Alisema baadhi ya watu hao wanaotishia maisha yake, wamekuwa wakitoa tiba za uongo na wengine ni wagonjwa, hivyo wanajua baada ya muda mfupi hawatakuwapo duniani.
Mchungaji Mwasapila alifafanua kuwa, hata akifariki, Mungu hawezi kutoa uwezo wake kwa watu hao, kwani anapenda watu wanyeyekevu.
"Ndugu zangu kutokana na hali hii ndio sababu mmesikia matangazo kuwa ni marufuku kunishika mkono ili mnisalimie, naomba muelewe hivyo," alisema Mwasapila.
Alisema miongoni mwa makundi yanayompinga, ni wachungaji wanaowakataza waumini wao kwenda kupata tiba Samunge wakihofia kukosa sadaka.
"Naomba mje mpate kikombe cha tiba na mkipona mkawape sadaka yao, najua hilo ndio tatizo lao," alisema Mwasapila.Awali, Msaidizi wa mchungaji huyo ambaye ni Ofisa wa Serikali, Frederick Nisajile, alitangaza kuwa sasa ni marufuku kumsalimia mchungaji bila idhini kutokana na sababu za usalama.
Apiga marufuku fulana kuandikwa jina lake
Katika hatua nyingine, Mchungaji Mwasapila jana alitangaza kupiga marufuku kampuni za ndani na nje ya nchi kuendelea kutengeneza fulana zenye picha yake na kuuza bila idhini yake.
Akizungumza na Mwananchi jana, Mchungaji Mwasapila huku akitazama baadhi ya fulana zenye jina lake na sura yake zilipelekwa kuuzwa Samunge, alisema anawaomba watu hao kuacha kutumia jina lake kujinufaisha.
"Naomba unisaidie kueleza kuwa kama kuna kampuni au watu wanataka kutumia jina langu na picha kwenye biashara zao wawasiliane na mimi kwanza, la sivyo vyombo vya dola vitawashughulikia," alisema Mwasapila.
Kuhusu fulana ambazo jana zilikuwa zinauzwa Samunge, alisema kwanza wametengeneza bila ridhaa yake, lakini picha wanazotumia kutengeneza fulana hizo hazina ubora.
"Waje hapa tuzungumze kuna ambao wamefika hapa na nimewapa utaratibu wa kufanya biashara yao nadhani tumeelewana,"alisema Mwasapila.
Fulana ambazo jana zilikuwa zikiuzwa Samunge, zilikuwa na picha ya mchungaji huyo na maneno mbalimbali ikiwamo 'Mchungaji wa ukweli wa Loliondo', 'Mtumishi wa Mungu Loliondo', 'Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokowae'.
HATA HIVYO KIKOMBE KINAENDELEA NA DAWA INACHEMKA KAMA KAWAIDA.....!