chikita

TANGAZA NASI

Tuesday, April 26, 2011

BURIANI SHELEMBI....! TULIKUPENDA SANA NA HATUTAKUSAHAU



                                    MAREHEMU PHILIPO SHELEMBI MAGADULA
"................mimi kwa jina naitwa Philipo Shelembi magadulla, ng'wanabyula, jembe na pia mashine ya kukoboa na kusaga mafisadi.......! ni mwenyekit  wa chadema mkoa wa Shinyanga, mjumbe wa halimashauri kuu ya chadema taifa na  vilevile ni mgombea wa ubunge kupitia chama hiki katika jimbo la Shinyanga...."
haya ni maneno ambayo niliyazoea kuyasikia mara kwa mara kila nilipohudhuria vikao vya bwana sherembi wakti akituomba kura za kuwa mbunge wetu mwaka 2010 na pia wakati akimnadi bwana Bob makani kwa vipindi viwili mfululizo yaani 2000 na 2005.
 kifupi nilimfahamu vizuri Mh sherembi maana wakati wa kampeni yake aliniomba niwe kampeni manager wa siri na tulikuwa tukifanya kampeni  za nyumba kwa nyumba hasa maeneo ya vijijini ambako tulikuwa tuna upinzani mkali kutoka ccm.
tulifanya nae mengi ila leo ninapopiga simu yake haipatikani na ninapoamini kwamba sitamuona tena sina ujanja zaidi ya kumuombea kwa Mungu apumzike kwa amani.
Mh, Sherembi umetusaidia sana Shinyanga katika kuleta Demokrasia ya ukweli, hatutakusahau
TUJIKUMBUSHE.

 mh Zitto kabwe akimnadi kwa wapiga kura Bwana Shelembi wakati wa uhai wake
 baada ya kumnadi ndipo aliamua kumpatia microphone ili naye aongee na wananchi. ndipo ailanza kama kawaida yake.

R.I.P