SERIKALI ya awamu ya nne iliingia madarakani na kauli mbiu ya
“Maisha bora kwa kila Mtanzania.” Timu ya wana mtandao iliyoiingiza hii
serikali ndani ya ikulu yetu, ilibobea katika uundaji wa kauli mbiu.
Itakumbukwa kuwa ni timu hiihii ya wana-mtandao iliyoibuka na kauli mbiu ya “Kasi mpya, Ari mpya na Nguvu mpya.” Hata baada ya mtandao kusambaratika, Rais Kikwete na mtandao masalia walikuja na kauli mbiu ya “Kasi zaidi, Ari zaidi na Nguvu zaidi.” Laiti mvuto wa kauli mbiu ungeendana na uhalisia; Watanzania tungekuwa mbali sana.
Watu wengi hivi sasa wanakubaliana pasipo kutumia vigezo maalum kuwa, chini ya serikali ya awamu ya nne, hali mbaya imekuwa na kasi, ari na nguvu zaidi kuliko mambo mazuri.
Tamko hili bila vigezo linaweza kuonekana ni propaganda za kisiasa, lakini kwangu mimi kigezo kikuu ni waasisi wenyewe wa kauli mbiu hizi ambao nimeongea nao na wao wakakiri kuwa, “Mambo yamegeuka kinyume na walivyotarajia.”
Hata ukitumia kipengele kimoja tu cha thamani ya shilingi ya Tanzania ambacho ni mhimili mkuu wa shughuli zote za kiuchumi ndani ya nchi, ni rahisi kuona ukweli wa hoja yangu.
Wakati serikali hii inaingia madarakani mwaka 2005, thamani ya shilingi dhidi ya dola ilikuwa kati ya Sh. 1,000 na 1,100. Hivi sasa shilingi imeporomoka sana na muda si mrefu yaweza kuingia shilingi 2,000 kwa dola moja hata kabla ya mwisho wa mwaka huu; huku mfumoko wa bei ukipaa.
Kutokana na kuporomoka kwa thamani ya shilingi, wiki hii tumeshuhudia matangazo ya kiama kwa Watanzania. TANESCO wametangaza ongezeko la bei ya umeme wakati hata mgawo wenyewe haujaisha.
Mamlaka ya Udhibiti Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza ongezeko la bei ya mafuta ya taa, petroli na dizeli. Ongezeko la bei ya mafuta linakuja wakati ambapo hata baadhi ya vituo vya mafuta vilikuwa bado vikiendelea na mgomo wa kuuza nishati hiyo. Ongezeko hili halitegemewi kuondoa mgomo huo kwa sababu linatokana na kuporomoka kwa thamani ya shilingi.
Inaeleweka vema kuwa ongezeko la bei ya umeme na mafuta linaongeza moja kwa moja bei za bidhaa nyinginezo pamoja na huduma muhimu za kijamii. Haitarajiwi kuwa ongezeko hili litaongeza ubora wa huduma wala kuzisogeza karibu na watumiaji. Kimantiki, ongezeko la bei kwa huduma hizi, ni ongezeko la maumivu kwa watumiaji.
Kama nilivyodokeza hapo juu, mtiririko wa matukio yanayofanya maisha ya Watanzania kuwa magumu, ni kinyume na matarajio ya wahandisi/wajenzi wa mfumo wa utawala wa serikali ya sasa. Hata wao wanashangaa ni kwa nini mambo yanazidi kuwa magumu. Kinachokosekana ni tamko lao hadharani kuwa hali ni ngumu.
Wanasema na kusononeka mafichoni wakati Watanzania waliowaweka madarakani wanazidi kuumia. Kwa hali ya uchumi kugeuka na kuwa kinyume na matarajio ni jambo la kawaida katika mifumo ya uchumi.
Kilicho kigeni katika hali yetu, ni tabia ya watawala kushindwa kueleza wazi ni nini kimetokea na kufanya hali za Watanzania kuzidi kuwa mbaya kuliko zilivyokuwa kabla hawajaingia madarakani. Badala ya kusema ukweli, watawala wamekazana kutangaza kuwa uchumi unapaa na hali ya Watanzania ni bora!
Kwa sasa kauli mbiu inayofaa ni ile ya “Maisha mabaya kwa kila Mtanzania.” Haiwezekani kwamba watawala wetu hawa walikaa, wakapanga kuwa walete maisha mbaya kwa kila Mtanzania. Lakini kutokana na kimya chao, hisia zinaanza kujengeka miongoni mwa Watanzania kuwa yawezekana walipanga hivyo. Hisia hizi zikiachwa ziaminike, itakuwa vigumu kudhibiti ghadhabu ya wananchi dhidi ya serikali hii.
Awamu iliyopita ilikabidhi mustakabali wa uchumi wa taifa letu mikononi mwa wawekezaji. Serikali iliuza kila kitu na kufungua milango yote kwa wawekezaji. Matokeo ya sera hii, wote tumeyaona kwa masikitiko makubwa sana.
Watanzania wamegeuka kuwa wapangaji na wapagazi huku wageni wakiwa wamiliki wa njia kuu za uchumi. Rais Mkapa aliwahi kunukuliwa akisikitika kuwa hali hii hakuikusudia kwa sababu alidai yeye alilenga “kubinafsisha” siyo “kubinafasisha.”
Chini ya serikali ya Mkapa, wawekezaji walipata ushirikiano mzuri wa serikali na kuwekewa mazingira ya kunyonya raslimali zetu; lakini pia kulikuwa na mwanya fulani kwa baadhi ya wazawa kufaidi kupitia migongo ya wawekezaji hao.
Mazingira ya wawekezaji kwa sasa yamebadilika. Sera za uchumi wa taifa letu hazieleweki na zinazoeleweka hazifuatwi. Serikali inayoimba wimbo wa uchumi wa soko huria, hivi sasa imetumbukia katika mkakati wa udikteta unaotishia usalama wa mitaji ya wawekezaji kwa sababu hakuna umeme wa uhakika.
Aidha, hakuna uhuru kamili wa kuendesha soko huria, hakuna mazingira sawa ya ushindani na wala hakuna dalili za kukomesha rushwa na ukiritimba katika shughuli za kiuchumi.
Mzunguko mzima wa shughuli za uwekezaji umejaa rushwa kila hatua na kutegeana. Mmoja wa wawekezaji wazoefu hapa nchini amenieleza kuwa kila hatua analazimika kuonana na rais ili aweze kufanya shughuli zake kwa ufanisi!
Watanzania wameshuhudia mijadala ya ajabu bungeni kuhusiana na masuala ya uwekezaji na uendeshaji wa shughuli za biashara. Huku katika upande mmoja bunge likionekana wazi kuingilia wajibu wa serikali na upande wa pili, bunge likinukia harufu ya udikteta pale lilipofikiria kutumia jeshi kulazimisha uuzwaji wa mafuta katika vituo vya mafuta.
Hizo ni dalili tosha kuwa “maisha mabaya” kwa kila Mtanzania yanaipeleka nchi kwenye eneo gumu kiutawala. Unapoona msajili wa vyama vya siasa akijiingiza kichwakichwa katika kampeini za kubeza maandamano ya vyama vya siasa, ujue “maisha mabaya” kwa kila Mtanzania yamefika hata ndani ya ofisi ya msajili wa vyama vya siasa na kumfanya aache kuwa refa na kuwa mchezaji kamili wa siasa za vyama.
Ni vema tukajiuliza mpaka hapa, ni taasisi gani haijaguswa na “maisha mabaya” kwa kila Mtanzania. Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi yaliingia mapema pale yalipoanza kutumiwa kama matawi ya chama tawala kutoa matamko elekezi.
Mahakama zilishirikishwa katika semina elekezi za watendaji wa serikali na kutoa viapo vya kuisaidia katika kukabiliana na wote wanaohoji kwa nini kuna “maisha mabaya” kwa kila Mtanzania.
Bunge ambalo ni chombo cha wananchi, limegeuka kuwa kama kinyonga. Mara tunaliona likitoa meno makali, lakini haichukui muda linanywea kama puto lililoishiwa pumzi.

Panahitajika kauli ya watawala juu ya tulipo sasa, kwa nini tuko
hapa; wamekwama wapi na tuchukue hatua gani kuondoa “maisha mabaya kwa
kila Mtanzania” ambayo yameingia katika kila kaya na maisha ya kila
mmoja. Kunyamaza hakutaondoa chuki ya wananchi.